Nenda kwa yaliyomo

Friday

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Friday
Image
Imeongozwa na F. Gary Gray
Imetayarishwa na Patricia Charbonnet
Imetungwa na Ice Cube
DJ Pooh
Nyota
Muziki na Frank Fitzpatrick
Simon Franglen
Chuck Wild
Imehaririwa na John Carter
Imesambazwa na New Line Cinema
Imetolewa tar. 26 Aprili 1995
Ina muda wa dk. Dakika 91
97 minutes (Director's cut)
Nchi Marekani
Lugha Kiingereza
Bajeti ya filamu $3.5 million
Mapato yote ya filamu $27.5 million

Friday ni filamu ya washikaji-ya-vichekesho ya mwaka wa 1995 kutoka nchini Marekani. Filamu imeongozwa na F. Gary Gray ikiwa ndiyo filamu yake ya kwanza kuongoza. Ndani yake anakuja Ice Cube, ambaye pia alishiriki katika kuandika muswaada andishi wa filamuna DJ Pooh, na Chris Tucker katika uhusika wake wa kwanza kwenye filamu. Filamu inaelezea masaa 16 ya maisha bila ajira ya Craig Jones (Cube) na Smokey (Tucker), ambaye anatakiwa alipe deni la dola 200 la mwuza dawa za kulevya ifikapo saa 4 kamili usiku huo.

Mafanikio ya filamu yamezaa matoleo mengine mawili: Next Friday (2000) na Friday After Next (2002). Sehemu ya nne ya filamu itaitwa Last Friday ilikuwa ikishuhulikiwa kwa miaka kadhaa sasa lakini imepitishwa mnamo mwezi wa Aprili 2017 - na hiyo ni kwa mujibu wa John Witherspoon.[1]

Craig Jones (Ice Cube), kijana mkazi wa Los Angeles, amepoteza kazi yake hivi karibuni baada ya kusingiziwa wizi. Akiwa hana mpango mwingine, anatumia siku yake katika kibaraza cha nyumba yao akiwa na rafiki yake, Smokey (Chris Tucker), ambaye ni muuzaji mdogo wa bangi anayemfanyia kazi Big Worm (Faizon Love), msambazaji mkatili wa dawa za kulevya mtaani hapo.

Siku nzima, Craig na Smokey wanashuhudia matukio mbalimbali ya majirani zao: Ezail, mraibu wa dawa za kulevya anayeishi kwa wizi mdogo; Debbie Parker (Nia Long), mwanamke anayevutiwa na Craig; Stanley, jirani mshamba wa mali zake; Red (DJ Pooh), rafiki wa zamani wa Craig ambaye baiskeli na mkufu wake viliporwa na Deebo (Tiny Lister Jr.), mbabe na mnyanyasaji wa mtaani; na Mchungaji Clever (Bernie Mac) ambaye ananaswa akizini na mke wa Bwana Parker.

Mgogoro mkuu unaanza wakati Smokey anapogundulika kuwa amevuta bangi aliyopewa kuuza badala ya kuingiza faida. Big Worm anagundua upotevu wa pesa na kumtishia Smokey, ambaye anamsingizia Craig kuwa amemsaidia kuvuta bangi hiyo. Big Worm anatoa onyo kuwa atawaua wote wawili iwapo hawatalipa pesa hizo ifikapo saa nne usiku.

Craig anajaribu kutafuta pesa kwa mama yake, dada yake, na mpenzi wake mwenye wivu, Joi, lakini anashindwa. Baba yake, Willie (John Witherspoon), anagundua kuwa Craig amebeba bunduki kwa ajili ya ulinzi. Willie anamshauri Craig kuweka silaha chini na kutumia mikono yake kutatua matatizo, akimkumbusha kifo cha ndugu yao kilichosababishwa na ghasia za bunduki.

Usiku unapokaribia, gari la wahuni wa Big Worm linapita mtaani na kuanza kushambulia kwa risasi. Craig na Smokey wanafanikiwa kujificha na kunusurika. Baadaye, Deebo anampiga Felisha (dada wa Debbie) na kisha kumshambulia Debbie mwenyewe baada ya kutokea ugomvi. Kitendo hiki kinamkasirisha Craig ambaye anaamua kumkabili Deebo.

Licha ya kutaka kutumia bunduki awali, Craig anakumbuka ushauri wa baba yake na kuweka silaha chini. Anaingia kwenye mapigano ya ana kwa ana na Deebo. Baada ya mapambano makali, Craig anampiga Deebo na kumwangusha kwa kutumia matofali na vifaa vingine kama silaha.

Baada ya ushindi huo, Red anachukua baiskeli yake na mkufu kutoka kwa Deebo aliyezirai, na Ezail anaiba viatu vyake. Smokey anachukua pesa alizokuwa akidaiwa na Big Worm kutoka kwenye mfuko wa Deebo na kumlipa mdai wake kupitia simu, huku akidai kuwa ameacha kutumia dawa za kulevya. Filamu inaishia hapo huku Smokey akivunja ukuta wa nne na kumwambia mtazamaji kuwa alikuwa anatania tu kuhusu kuacha bangi.

Washiriki

[hariri | hariri chanzo]
  1. EURPublisher01. "John Witherspoon: Ice Cube Says New 'Friday' Movie Has Studio Greenlight". EURweb. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-04-22. Iliwekwa mnamo 2017-04-27.{{cite web}}: CS1 maint: numeric names: authors list (link)

Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]
Image
Wikiquote ina mkusanyiko wa dondoo kuhusu: