Nimepokea kwa mikono miwili maamuzi ya uchaguzi wa Mkutano Mkuu wa Chama chetu CHADEMA uliohitimishwa leo asubuhi 22 Januari 2025. Nampongeza Mhe. Tundu Lissu na wenzake kwa kuaminiwa kutwikwa jukumu la Uongozi wa Chama. Nawatakia kila la kheri katika kukipeleka mbele Chama
Nimewasikiliza Wah Rais JPM na Spika Job Ndugai. Nimesikitika! Tunatafakari! Nitazungumza tena na Taifa wakati wowote! Ni maisha yetu. Viongozi wetu waelewe: Hatuhitaji kibali chao kufa. Kuishi ni haki yetu. Tukumbuke: Tujilinde. Tuliowategemea wako likizo na Corona sio siasa.
Shambulio la Polisi wa Nyamongo, Tarime dhidi ya Mgombea U-Rais, Wabunge, Viongozi, Wanachama na Wapenzi wa Chadema ni uchokozi usiokubalika. Risasi za Moto na Mabomu yanatonesha vidonda na makovu yetu ya miaka mingi. IGP usiruhusu tabia hii kuendelea. Italigharimu Taifa.
Watanzania wenzangu, tuna masaa 24 kwa NEC kuweka Msingi wa Amani ya Tanzania. Mkakati wowote wa kuengua kwa hila wagombea wetu utapokelewa kwa kishindo kikubwa. #NoLissuNoElection!#SasaBasi! Uzalendo uonyeshwe kwa kusimamia haki na si vinginevyo.
Kesho & kila J’mosi nitavaa SARE ZA CHAMA CHETU CHADEMA hadi TZ ipate KATIBA MPYA. Azimio hili limependekezwa & kuungwa mkono & Vikao & Mikutano yote inayoendelea nchini. WANACHADEMA wote tuungane, tutambuane, tukilinde Chama & tutetee Uhuru na Haki popote tulipo. Umoja ni nguvu!
That’s my Dad! That’s our history! Thank you Dad. You fought for our country independence. I am now fighting for our Country Freedom, Justice and Development!!
Kesho J3, 14/6/21 asubuhi, nitaungana na Familia ya CHADEMA katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya kusikiliza hukumu ya kesi inayomkabili Mdude Nyagali. Mdude amepitia miaka 5 ya mateso na uonevu usio kifani. Ataheshimishwa kwa kuisimamia Imani! Naamini haki itatendeka.
Kuna uvurugwaji wa kutisha wa Daftari la wapiga kura. Mamilioni ya wapiga kura hewa & maelfu ya vituo bandia. Wapiga kura wengi wapinzani wamehamishwa vituo au kuondolewa kwa makusudi. NEC itoe maelezo & suluhisho haraka la sivyo uchaguzi huu utashindikana kuanzia hatua ya awali.