Nenda kwa yaliyomo

Maldivi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
ދިވެހިރާއްޖޭގެ ޖުމުހޫރިއްޔާ
Jamhuri ya Maldivi
Bendera ya Maldivi Nembo ya Maldivi
Bendera Nembo
Kaulimbiu ya taifa:
Wimbo wa taifa: Gavmii mi ekuverikan matii tibegen kuriime salaam
"Twasalimu taifa letu kwa umoja"
Lokeshen ya Maldivi
Mji mkuu Malé
4°10 N 73°30 E
Mji mkubwa nchini Malé
Lugha rasmi Kidhivehi, Kiingereza
Serikali Jamhuri
Mohamed Muizzu
Uhuru
kutoka Uingereza
26 Julai 1965
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
298 km² (ya 187)
--
Idadi ya watu
 - [[]] kadirio
 - 2022 sensa
 - Msongamano wa watu
 
(ya 1671)
515,132
1,728.63/km² (ya 7)
Fedha Rufiyaa (MVR)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
(UTC+5)
(UTC)
Intaneti TLD .mv
Kodi ya simu +960

-

1 Makadirio ya UM ya 2005.


Image
Malé ni mji mkuu wa Maldivi

Maldivi (jina rasmi: Jamhuri ya Maldivi; Kidhivehi: ދިވެހި ރާއްޖެ) ni nchi ya visiwa iliyoko Asia Kusini katika Bahari ya Hindi, kusini-magharibi mwa Sri Lanka na India. [1] Kufikia mwaka 2024, inakadiriwa kuwa na idadi ya watu takriban 520,000, ikiwa miongoni mwa nchi ndogo zaidi barani Asia kwa idadi ya watu na eneo la ardhi. Mji mkuu na mkubwa ni Malé, huku nchi ikiwa imegawanywa katika atoli 20 za kiutawala na lugha rasmi ikiwa Kidhivehi. [2]

Kabla ya uhuru ilikuwa chini ya ulinzi wa Uingereza tangu mwaka 1887. Kwa jumla kuna visiwa 1,196 na kati ya hivyo takriban 200 hukaliwa na watu.

Wakazi karibu wote (98.7%) ni Waislamu, hasa Wasuni; ya kwao ndiyo dini rasmi na ya lazima kwa raia wote. Wakristo ni 0.29% (nusu Wakatoliki na nusu Waprotestanti).

Lugha ya kawaida na lugha rasmi ni Kidhivehi, mojawapo ya lugha za Kihindi-Kiulaya.

Maldivi iko hatarini kupotea. Ni kwamba kimo cha juu cha nchi yake ni mita 5.1 pekee juu ya uwiano wa bahari, na wastani wake ni mita 1.5 tu. Hivyo, kama mabadiliko ya hali ya hewa kutokana kwa kupanda kwa halijoto duniani yatazidi kuleta kupanda kwa uwiano wa bahari, nchi hii yote itazama chini ya maji.

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  1. "Maldives - World Factbook: Geography". cia.gov. Central Intelligence Agency. Aprili 2026. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2022-07-28. Iliwekwa mnamo Mei 31, 2026.
  2. Clarence Maloney (Machi 25, 2026). "Maldives". Britannica. Iliwekwa mnamo Mei 31, 2026.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Nchi na maeneo ya Asia

Afghanistan | Armenia2 | Azerbaijan | Bahrain | Bangladesh | Bhutan | Brunei | China | Falme za Kiarabu | Georgia2 | Hong Kong3 | Indonesia | Iran | Iraq | Israel | Jamhuri ya China (Taiwan) | Japani | Kamboja | Kazakhstan | Kirgizia | Korea Kaskazini | Korea Kusini | Kupro2 | Kuwait | Laos | Lebanoni | Macau3 | Malaysia | Maldivi | Mongolia | Myanmar | Nepal | Omani | Pakistan | Palestina | Qatar | Saudia | Singapuri | Sri Lanka | Syria | Tajikistan | Timor ya Mashariki | Turkmenistan | Ufilipino | Uhindi | Urusi1 | Uthai | Uturuki1 | Uzbekistan | Vietnam | Yemen | Yordani

1. Nchi ina maeneo katika Asia na Ulaya. 2. Nchi iko Asia lakini inahesabiwa pia kati ya nchi za Ulaya kwa sababu za historia au utamaduni. 3. Eneo la pekee la China.
Image Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Maldivi kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.